← Soma kwa Kiingereza / Read in English
AFYA YA MMENG'ENYO WA CHAKULA · DAKIKA 6 ZA KUSOMA

Tofauti na Inavyodhaniwa na Wengi, Vidonda vya Tumbo Vinatibika!

Kopo la dawa lishe ya mimea HAIIBA IG Gel kutoka Herbal Impact kwa ajili ya vidonda vya tumbo
READ IN ENGLISH

Watu wengi wanaamini kuwa vidonda vya tumbo ni ugonjwa wa kudumu usiopona. Ukweli ni kwamba vidonda vya tumbo vinatibika — kama chanzo chake kitajulikana na matibabu yatafuatwa kikamilifu.

H. Pylori: Bakteria Anayesababisha Vidonda vya Tumbo

*Helicobacter pylori*, au kwa kifupi H. pylori, ni bakteria anayetajwa kuwa chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo. Maambukizi yake mara nyingi hutokea utotoni, pale watoto wanaposhindwa kuzingatia kanuni za usafi. Bakteria huyu akishaingia mwilini anaweza kuishi kwenye mfumo wa usagaji chakula kwa miaka mingi bila kuonyesha dalili yoyote.

Mtu anaweza pia kuambukizwa kupitia:

Tafiti za kimataifa zinakadiria kuwa karibu nusu ya watu wote duniani wana maambukizi ya H. pylori. Viwango viko juu zaidi katika jamii ambazo mifumo ya maji safi na maji taka haijaimarika.

Kwa Nini Si Kila Aliyeambukizwa Hupata Vidonda?

Wengi wenye H. pylori hawapati dalili zozote. Inakadiriwa kuwa ni kati ya mtu 1 kati ya 10 hadi 1 kati ya 5 tu ya walioambukizwa ndio huishia kupata vidonda vya tumbo. Hadi sasa wanasayansi hawajajua kwa uhakika kwa nini baadhi hupata vidonda na wengine hawapati.

Jinsi H. Pylori Anavyozalisha Vidonda

Ndani ya tumbo kuna utando (stomach lining) unaolinda tishu dhidi ya tindikali inayotumika kusaga chakula. H. pylori hudhoofisha utando huu — ndani ya mfuko wa tumbo au kwenye sehemu ya mwanzo ya utumbo mwembamba inayoungana na tumbo. Utando ukishaharibika, tindikali hupenya na kufikia tishu. Tishu hizo hupata mfuro (inflammation), na mfuro huo huzaa vidonda.

Vidonda visipotibiwa vinaweza kusababisha damu kuvuja tumboni, maambukizi ya ziada, au kuzuia chakula kupita vizuri kwenye mfumo wa usagaji chakula.

Dalili za Vidonda vya Tumbo

Ukiwa na dalili zifuatazo, kuna uwezekano mkubwa kuwa una maambukizi ya H. pylori ambayo yameanza kuzaa vidonda:

1. Tumbo kujaa gesi (bloating)

2. Kupiga mbweu mara kwa mara

3. Kichefuchefu na kutapika

4. Kujisikia vibaya tumboni (stomach discomfort)

5. Kukosa hamu ya kula

6. Kupungua uzito bila sababu ya msingi

7. Kiungulia

8. Harufu mbaya kinywani

Dalili za Hatari: Nenda Hospitali Mara Moja

Vidonda vikiwa katika hali mbaya zaidi vinaweza kuzaa dalili nzito kama:

1. Maumivu makali ya tumbo

2. Kutapika matapishi yenye damu

3. Haja kubwa yenye damu au nyeusi kama lami

4. Kizunguzungu

5. Shida ya kupumua

6. Uchovu usio na sababu

Ukiwa na dalili hizi, fika hospitali haraka.

Pima Kwanza Upate Uhakika

Ukiwa na baadhi ya dalili hizi, au zote kwa pamoja, nenda hospitali kufanya vipimo. Sababu kubwa ni kupata uhakika, kwani ziko sababu nyingine zinazoweza kuzaa dalili kama hizi.

Kwa mfano, mtu anayetumia dawa za maumivu za jamii ya NSAIDs (Non-Steroidal Anti-Inflammatory Drugs) kama ibuprofen, diclofenac na aspirin anaweza kupata vidonda pia. Tafiti zinaonyesha kuwa NSAIDs, kama ilivyo kwa H. pylori, hushambulia na kuumiza utando wa ndani wa tumbo.

H. pylori pia ametambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama chanzo kinachoongeza hatari ya saratani ya tumbo. Hii ni sababu nzuri ya kuchangamkia matibabu mapema pale unapogundulika kuwa na vidonda vya tumbo.

Tiba ya Hospitali: Kwa Nini Wengi Hawapone?

Maambukizi ya H. pylori hutibiwa hospitalini kwa mchanganyiko wa viuavijasumu (antibiotics) kama amoxicillin, tetracycline na metronidazole (Flagyl). Hata hivyo, uzoefu unaonyesha kuwa kumwangamiza bakteria peke yake hakutoshi kuponya vidonda ambavyo tayari vimeshatokea.

Ili vidonda vipone kabisa, matibabu lazima pia yadhibiti tindikali tumboni pamoja na mfuro kwenye vidonda. Ndiyo maana tiba ya hospitali huhusisha pia dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali, pamoja na dawa zinazozuia kemikali iitwayo histamine, ambayo pamoja na kazi nyingine huchochea tumbo kuzalisha tindikali.

Matibabu haya huchukua wiki kadhaa na yanahusisha kumeza vidonge vingi kila siku. Huenda hii ndiyo sababu kubwa inayofanya wengi wasipone: tulio wengi hukatiza dozi mara tunapohisi nafuu. Kama umeanzishiwa dozi, imalize yote kama ulivyoelekezwa na daktari.

Vidonda Vimekataa Kupona? Tembelea Herbal Impact

Kama una vidonda vya tumbo ambavyo unahisi vimeshindikana kupona kwa sababu yoyote ile, karibu Herbal Impact. Dawa lishe yetu ya mimea, HAIIBA IG, imekuwa msaada mkubwa kwa wateja wetu wengi wenye vidonda vya tumbo — wengi wao wakiwa wamehangaika kwa muda mrefu kabla ya kuanza kuitumia. Tunashauri kuitumia sambamba na ushauri wa daktari wako.

Wasiliana nasi:

Unataka kujua bidhaa zetu nyingine? Pakua bure Mwongozo wa Bidhaa na Huduma za Herbal Impact.

Onyo la kiafya: Makala hii ni kwa ajili ya taarifa za jumla za afya tu. Si ushauri wa kitabibu na hailengi kutambua, kutibu, kuponya au kuzuia ugonjwa wowote. Daima wasiliana na mtaalamu wa afya aliyehitimu kabla ya kuanza dawa au tiba yoyote mpya.

← Rudi kwenye makala zote / Back to all articles