← Soma kwa Kiingereza / Read in English
AFYA YA KINYWA · DAKIKA 4 ZA KUSOMA

Jinsi ya Kutunza Afya ya Kinywa kwa Uhakika

Mwanaume anayetabasamu akipiga mswaki, mfano wa kutunza afya ya kinywa, meno na fizi kila siku
READ IN ENGLISH

Afya ya kinywa inajumuisha maeneo mengi, lakini tunaweka mkazo kwenye meno na fizi kwa sababu matatizo yanayoyakumba maeneo haya ndiyo yaliyozoeleka.

Mwanaume anayetabasamu akipiga mswaki kutunza afya ya kinywa
Kupiga mswaki, hasa usiku kabla ya kulala, ni msingi wa afya ya kinywa. Picha: Tima Miroshnichenko / Pexels

Sababu Kuu Nne za Matatizo ya Meno na Fizi

Mara nyingi matatizo katika maeneo haya yanatokana na sababu kuu nne:

  1. Maambukizi ya Gram Positive Bakteria
  2. Mwili kuelemewa na tindikali
  3. Kushindwa kudhibiti kisukari kwa wagonjwa wa kisukari
  4. Upungufu wa vitamin C

Nafasi ya Gram Positive Bakteria

Mabaki ya vyakula na vinywaji katika vinywa vyetu ni kama sumaku kwa hawa bakteria. Bakteria hawa ndio wanaohusika na kupekecha meno na kuyafanya yawe na matundu.

Aidha bakteria hawa ndio wanaohusika na kuambukiza fizi na kuzifanya zikumbwe na mfuro (inflammation), na hatimaye kupelekea uharibifu wa hizo tishu.

Hata hivyo kuwadhibiti hawa bakteria ni rahisi sana kwa sababu kinachohitajika ni usafi wa uhakika wa kinywa.

Kimsingi tunapaswa kupiga mswaki kila baada ya kula na kunywa. Hata hivyo kutokana na ugumu wa mazingira tunapaswa kufanya hivyo japo mara mbili kwa siku (asubuhi na usiku kabla ya kulala); ila tunapaswa kuzingatia kuwa kupiga mswaki usiku kabla ya kulala ni bora zaidi kuliko kupiga asubuhi.

Nafasi ya Tindikali

Zaidi ya 50% ya miili yetu ni majimaji.

Majimaji haya ambayo yanapatikana katika maeneo mbalimbali ya mwili, ukiondoa katika mfuko wa tumbo, yanapaswa kuwa katika hali ya ualkali (kitaalamu pH zaidi ya 7.0).

pH ya 7.0 ni pH ya maji, na pH chini ya 7.0 ni pH ya tindikali.

Hata hivyo kwa bahati mbaya majimaji haya yaliyoko mwilini hugeuka taratibu na kuwa katika hali ya utindikali kutokana na lishe ya protini na wanga, msongo wa akili, pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na mwili.

Mwili unapokuwa katika hali ya utindikali ni habari mbaya.

Hali hii husababisha mabadiliko hasi katika mifumo mingi ya mwili, ikiwa ni pamoja na mifupa kupoteza madini ya calcium (kalisi).

Meno ni mifupa pia, hivyo mwili ukiwa na tindikali nyingi yanadhoofika na kuanza kumeguka. Aidha yanatoa nafasi kwa Gram Positive Bakteria kufanya kazi ya upekechaji kwa wepesi.

Lishe Bora kwa Afya ya Kinywa: Kanuni ya 80/20

Ili kuondokana na hali hii tunapaswa kuzingatia sana lishe yetu. Inapendekezwa kula kwa kuzingatia kanuni ya 80/20.

Kanuni hii huelekeza kuwa asilimia 80 ya sahani yako ya mlo iwe ni mbogamboga mchanganyiko, na ikiwezekana 75% ya hizo mbogamboga ziwe ghafi (raw).

Mbogamboga na matunda ndivyo vyakula pekee vyenye madini ya alkali ambayo ni muhimu sana katika kuzimua tindikali mwilini ili isisababishe madhara.

Kutokana na matunda kuwa na sukari nyingi ambayo ni rahisi kuchachuka kama yatabaki katika mfuko wa tumbo kwa muda mrefu, inashauriwa matunda yaliwe peke yake, na walau iwe nusu saa au zaidi kabla ya mlo wa kawaida.

Nafasi ya Kisukari

Kisukari ambacho hakijadhibitiwa hufanya uharibifu mkubwa katika mfumo wa mzunguko wa damu, na kusababisha damu ishindwe kufika katika baadhi ya tishu za mwili.

Hali hiyo hupelekea tishu hizo kukumbwa na uhaba mkubwa wa viinilishe pamoja na hewa ya oksijeni.

Moja ya maeneo yanayoweza kuathiriwa sana na kisukari ni fizi. Fizi zilizoathiriwa zinakuwa dhaifu na hupelekea meno kulegea na hata kung'oka hovyo.

Nafasi ya Vitamin C

Tishu zinazounda fizi ni miongoni mwa zile zinazoitwa connective tissues. Hizi ni zile ambazo kazi yake kuu ni kutoa sapoti, kushikilia na kuunganisha viungo vingine.

Connective tissues zinahitaji protini inayoitwa collagen ili zitengenezeke kikamilifu. Bila vitamin C mwili hauwezi kuzalisha collagen.

Ukiwa na upungufu mkubwa wa vitamin C, connective tissues mbalimbali ndani ya mwili zitadhoofika ikiwa ni pamoja na fizi. Dalili kwamba fizi zako zina athari hii ni kutoa damu.

Vitamin C inapatikana kwenye mbogamboga mbalimbali na matunda mengi. Matumizi ya matunda kama ndimu na malimao ni njia ya gharama nafuu ya kupata kiwango cha kutosha cha vitamin C ndani ya mwili kila wakati.

Haiiba Dental Guard kwa Maumivu ya Meno

Kama una maumivu ya meno na usingependa kung'oa unaweza kuwasiliana nasi kupata dawa inayoitwa Haiiba Dental Guard.

Dawa hii huua mamilioni ya gram positive bakteria kwa kugusana tu. Matumizi ya dawa hii huondosha maumivu ya meno ndani ya dakika 15 hadi 20, na aghalabu maumivu hayo hayarejei tena.

Dawa hii pia hutibu magonjwa ya fizi yanayotokana na maambukizi na hivyo kuwa tiba bora kwa kinywa kinachotoa harufu mbaya kutokana na uharibifu wa tishu za fizi.

Je, Ungependa Kupata Haiiba Dental Guard?

Agiza mtandaoni: payhip.com/b/hxvAR

AU

Tupigie/WhatsApp 0754 281 131 / 0655 281 131

AU

Tutembelee: mtaa wa Mosque, Kitumbini, Dar es Salaam (mkabala na msikiti wa Sunni).

Herbal Impact ni kliniki ya tiba asili na tiba mbadala iliyosajiliwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania. Kama uko kwenye matibabu ya hospitali, endelea nayo na mjulishe daktari wako kuhusu dawa za asili unazotumia.

Onyo la kiafya: Makala hii ni kwa ajili ya taarifa za jumla za afya tu. Si ushauri wa kitabibu na hailengi kutambua, kutibu, kuponya au kuzuia ugonjwa wowote. Daima wasiliana na mtaalamu wa afya aliyehitimu kabla ya kuanza dawa au tiba yoyote mpya.

← Rudi kwenye makala zote / Back to all articles